SAKHO AWASHUKURU WATANZANIA,AKABIDHIWA TUZO NA OKOCHA

HATIMAYE staa wa Simba na raia wa Senegal,Pape Sakho bao lake alilofunga mbele ya ASEC Mimosas limeweza kupenya na kuwa bao bora la CAF.

Hatua hiyo imekuja baada ya mchujo mkali kwa kupitia kura na Julai 21 aliweza kutangazwa mshindi kwa kuwashinda washindani wake ambao aliingia nao tatu bora.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo nchini Morocco ambapo aliweza pia kukutana na staa Sadio Mane raia Pape amesema:-“Asanteni Watanzania, asanteni mashabiki wa Simba, asanteni wachezaji wote, nimefurahi sana.”

Sakho baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Bao Bora la CAF alikabidhiwa tuzo hiyo nchini Morocco na Legend wa mpira barani Afrika Jay Jay Okocha

Ikumbukwe kwamba bao hilo alipachika kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Uwanja wa Mkapa mbele ya ASEC Mimosas na Simba ilishinda mabao 3-1.

 Ni Zouhair El-Moutaraji  alifunga kwenye mchezo wa Wydad vs Al Ahly na Gabadinho Mhango mchezo wa Malawi vs Morocco hawa walikuwa ni washindani wake.