KAMBI YA YANGA RAMANI INACHORWA HIVI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kwa sasa wanafanya vikao kuweza kujadili wapi wataweka kambi kwa msimu wa 2022/23.

Awali mpango namba moja wa Yanga kuweka kambi ulipaswa kuwa nchini Uturuki lakini umeyeyuka ghafla kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni muda kuwa mdogo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga,Hassan Bumbuli ameweka wazi kuwa kambi lazima ifanyike kwa namna yoyote ila ni mpaka vikao vitakapoamua.

“Suala la kambi lipo na ni lazima iwe hivyo kwa namna yoyote ile awali tulitarajia iwe nchini Uturuki lakini baada ya vikao tutajua wapi kambi itakwenda kufanyika.

“Kikubwa mashabiki wasiwe na mashaka mipango inakwenda sawa na itajulikana hivi karibuni wapi kambi itakuwa kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23,”.

Yanga ni mabingwa wa ligi kwa msimu wa 2021/22 ambapo walitwaa ubingwa huo uliokuwa mikononi