RASMI uongozi wa Klabu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara umethibitisha kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo kwa msimu wa 2021/22.
Ikumbukwe kwamba Januari 11,2021 uongozi wa Polisi Tanzania ulibainisha kuwa kocha huyo Malale Hamsini ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo baada ya taarifa kuripotiwa kwamba amefutwa kazi.
Hatimaye yametimia leo Julai 2022 18 baada ya taarifa kutoka Polisi Tanzania kueleza kuwa wamefikia makubaliano ya kuachana na kocha huyo mzawa.
Taarifa iliyotolewa na Frank Lukwaro ambaye ni Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano imeeleza kuwa wamefikia makubalino ya kutoendelea na Malale katika msimu ujao wa 2022/23.
Kuhusu mrithi wa mikoba yake anatarajiwa kutangazwa hivi karibuni.
Msimu wa 2021/22 Malale Hamsini aliongoza timu hiyo kwenye mechi 30 na ilikusanya pointi 37 ikiwa nafasi ya 8 na aliwahi kutwaa tuzo ya kocha bora mwezi Septemba.