UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa hauna uhakika na mchezaji huyo kubaki ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao kutokana na uwezo alionao kwenye mikono yake na akili ya mpira.
Raia huyo wa Mali anaitwa Diarra Djigui huku jina la utani wakimuita ‘Screen Protector’ kutokana na kazi yake anayofanya akiwa kwenye lango.
Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa kwa namna kijana huyo anavyofanya kazi kubwa akiwa uwanjani hana imani kama anaweza kubaki Yanga.
“Sijui kama Diarra atabaki Yanga kwa kuwa amekuwa kwenye ubora mkubwa, macho yake na masikio yake ni ya kimpira muda wote na mpaka basi zake pia ni za uhakika.
“Usajili wake wengi waliubeza lakini kwa sasa ninaona kwamba wengi wanaona kuna kitu ambacho kipo. Usajili wetu ulikuwa ni mzuri na umeleta wachezaji wazui na bora,” alisema Manara.
Kwenye ligi akiwa amecheza mechi tano Diarra amekusanya clean sheet nnne akifungwa bao moja na Shaban Msala wa Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa.