KIPA namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya kwa msimu wa 2021/22 amekaa langoni kwenye mechi 9 za ligi ambapo aliweza kufungwa kwenye mechi tatu.
Tupo naye kwenye mwendo wa data kuangalia kile ambacho alikifanya katika kutimiza majukumu yake namna hii:-
Dk 540 za ushujaa
Kwenye mechi 6,Kakolanya alikuwa shujaa kwa kuweka lango salama ambapo hakuweza kutunguliwa ilikuwa:-
Biashara United
Dodoma Jiji
Polisi Tanzania
Mbeya City
Mtibwa Sugar
Mbeya Kwanza
Dk 270 za joto ya jiwe
Mechi tatu, Kakolanya aliweza kuonja joto ya jiwe namna hii na ilikuwa ni bao mojamoja:-
Geita Gold
Tanzania Prisons
KMC
Bao la kufungwa kwa penalti 0
Kadi nyekundu 0