KIKOSI cha Yanga kinachopewa minu na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo kimetwaa taji la Kombe la Azam Sports Federation maarufu kama FC kwa ushindi wa penalti mbele ya Coastal Union.
Ilikuwa ni fainali moja yenye ushindani mkubwa ndani ya dk 120 ambapo ubao wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ulikuwa unasoma Yanga 3-3 Coastal Union.
Ni mabao ya Abdul Seleman,’Sopu’ yeye aliweza kufunga yote matatu kwa Coastal Union huku kwa Yanga ni Feisal Salum.Heritier Makambo na Dennis Nkane hawa walifunga mabao kwa Yanga.
Ushindi wao Yanga leo ni wa penalti 4-1 ambapo kwa Coastal Union ni Victor Akpan pekee aliweza kufunga penalti hiyo