MCHEZO wa hatua ya nusu fainali, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa sasa ni mapumziko huku timu zote zikipambana kuweza kusepa na ushindi.
Ubao unasoma Yanga 0-1 Coastal Union chini ya kocha mzawa Juma Mgunda.
Bao la kuongoza kwa Coastal Union limepachikwa kimiani na Abdul Suleiman,’Sopu’ ambaye anafikisha mabao 7 kwenye Kombe la Shirikisho msimu huu.
Kwa upande wa Yanga kinara wa mabao ni Heritier Makambo mwenye mabao matatu