KLOPP BADO ANAMKUMBUKA MANE

JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool anaamini kwamba kuondoka kwa Sadio Mane ni jamo gumu kwake kwenda nalo sawa kwa sasa.

 Mane raia wa Senegal sasa atakuwa ni mali ya Bayern Munich baada ya timu hiyo kukamilisha usajili wake.

Unakuwa ni usajili wa tatu kwa Bayern Munich kukamilika ambapo Mane anakwenda kuchukua mikoba ya Robert Lewandowski ambaye anatarajia kuondoka kwenye kikosi hicho.

Klopp amesema:”Ni ngumu kusema kwamba ni mchezaji wa kawaida hasa ukizingatia tumekuwa naye kwa muda mrefu na anachofanya kinaonekana.

“Kwa sasa inakuwa ni kazi kuweza kumtafuta mwingine lakini ni moja ya wachezaji wazuri ambao wameondoka kwenye kikosi,”.