KUMTOA BEKI HUYU AZAM FC, JIPANGE KWELIKWELI

MABOSI wa Simba na Yanga kwa sasa ikiwa watakuwa wanahitaji kupata saini ya beki wa kazi ndani ya kikosi cha Azam FC,Daniel Amoah lazima wajipange kwa kuwa amejifunga miaka mingine zaidi.

Novemba 4, Amoah ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, George Lwandamina aliongeza dili la miaka miwili hivyo ataendelea kuwa ndani ya Azam Complex.

Mkataba huo alisaini mbele ya Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin, ‘Popat’ hivyo atadumu mpaka 2024.

Ndani ya Ligi Kuu Bara beki huyo ametupia bao moja kati ya manne yaliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya nane kwenye msimamo na pointi 7.