KIKOMBE CHA UBINGWA KILIACHWA MAPEMA,MIPANGO MUHIMU

 LIGI Kuu Tanzania Bara kwa sasa zimebaki mechi tatu kwa baadhi ya timu na nyingine zikiwa zimebakiwa na mechi mbili kukamilisha mzunguko wa pili.

Inaonekana kwamba ilikuwa ligi ngumu na yenye ushindani mkubwa ambapo kila timu ilikuwa inapambana kufanya vizuri tangu mwanzo wa msimu.

Hapa kuna picha nzuri ambayo imeweza kutengenezwa hasa kwenye upande wa timu ambazo zinakwenda kushuka daraja.

Mpaka sasa hakuna timu yenye uhakika wa moja kwa moja kwamba inaweza kubaki kwenye ligi ama kushuka kwa zile ambazo zipo kwenye nafasi tano za mwisho.

Ugumu huu umetokana na timu zote kuweza kufanya vizuri kwenye mechi za mzunguko wa kwanza lakini kwenye vita ya ubingwa kikombe kilikimbiwa mapema.

Kwa msimu ujao itapendeza ikiwa hivi kuanzia bingwa mpaka yule ambaye anakwenda kushuka ili uonyesha ukomavu kwenye msako wa pointi tatu.

Nina amini kwamba hesabu zikianza mzunguko wa kwanza kwa kila timu kushinda mechi zake hiyo itafanya kila mmoja kuzidi kuwa bora.

Kwa wale ambao wapo kwenye hatari ya kushuka daraja wana kazi moja ya kuweza kupambana ili kujinusuru kwenye mechi hizi za mwisho.

Ila hakuna namna lazima mbili ziweze kushuka hivyo zina jukumu la kuweza kuanza kujipanga upya kwa wakati ujao ikizwa zitashuka.

Kwa ambazo zitapanda zina kazi kubwa ya kuweza kujipanga kuweza kuwa bora wakati ujao ili kuweza kuepuka suala la kushuka daraja.

Ipo wazi kwamba Yanga imetwaa ubingwa mapema ikiwa na mechi mkononi hili ni jambo la kupongezwa kwao.

Mabingwa watetezi Simba wameweza kuona ile kasi ya watani zao wa jadi hivyo wana kazi ya kuweza kujipanga kwa wakati ujao.

Azam FC,Geita Gold mpaka Mbeya City zote zina nafasi ya kuweza kujipanga upya na kufanya vizuri zaidi wakati ujao.

Imeandikwa na Dizo Click.