RALLY Bwalya kiungo wa Simba amesema kuwa miaka miwili aliyodumu hapo amejifunza mengi kwa kuwa amefanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Jana Bwalya alicheza mchezo maalumu wa ligi na kuagwa kwa heshima na wachezaji pamoja na mashabiki wa timu hiyo ambayo ipo chini ya Seleman Matola ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo.
Kwenye mchezo huo jana wakati Simba ikishinda mabao 3-1 dhidi ya KMC ni mabao ya Pape Sakho,Kibu Dennis na Henock Inonga huku lile la KMC lilifungwa na Hassan Kabunda.
Bwalya amesema:”Kwa muda ambao nimekaa hapa nitawakumbuka mashabiki wa Tanzania kwa kuwa wamekuwa pamoja na sikwenye mafanikio ambayo tumeyafanya hilo lipo wazi.
“Kikubwa ulikuwa ni muda mzuri na tumefanya mambo kwa ushirikiano mzuri katika mafanikio ambayo tumeyafanya,hili ni jambo kubwa,” amesema.
Kiungo huyo mwenye pasi tatu na bao moja kwenye ligi anatajwa kuibukia Amazulu ya Afrika Kusini.