BAADA ya Said Ntibanzokiza kuachana na Yanga kocha wa makipa wa zamani wa timu hiyo Vladimir Niyonkuru raia wa Burundi ameweka wazi kuwa anatamani kumuona kiungo huyo akisaini Simba.
Saido mkataba wake ulimeguka Mei 30 na Yanga waliweka wazi kwamba wanamtakia kila la kheri kwenye changamoto mpya ambayo atakuwa kwa wakati ujao.
Kocha huyo amesema:”Nimesikia kwamba Saido kuna timu ambazo zinamuhitaji ikiwa ni pamoja na Singida Big Star (zamani ilikuwa ni DTB) pamoja na Simba hivyo ningependa aweze kusaini Simba,” amesema.
Kwa sasa Saido yupo huru na amekuwa akitumika kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Burundi inayowania kuwania tiketi ya kufuzu Afon.