IMEELEZWA kuwa mabosi wa Singida Big Stars wapo kwenye hesabu za kuoresha kikosi chao na wataanza kuwavuta nyota wenye uzoefu katika kikosi hicho.
Singida Big Stars imepanda daraja kutoka Championship ambapo kwa sasa ipo kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2022/23 ndani ya Ligi Kuu Bara na itatumia Uwanja wa Liti,Singida.
Dickson Ambundo,Deus Kaseke,Paul Godfrey,Erick Johora kutoka Yanga wanatajwa kuwa kwenye hesabu za timu hiyokwa ajili ya kufanya kazi kwenye timu hiyo ambayo imebadili jina kutoka DTB.
Wengine ni Said Ndemla anayekipiga Mtibwa Sugar kwa mkopo akitokea Simba,Yusuph Mhilu na Pascal Wawa kutoka Simba.