UBINGWA WA 28 WANUKIA LEO YANGA

JUNI 15, Uwanja wa Mkapa saa 2:30, Yanga v Coastal Union ni mchezo wa mzunguko wa pili ule wa kwanza Uwanja wa Mkwakwani, ubao ulisoma Coastal Union 0-2 Yanga.

Mchezo wa leo ikiwa Yanga itashinda itafikisha pointi 67 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu nyingine hivyo itakuwa imeshatwaa ubingwa wa ligi.

Ikitokea ikapoteza utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Yanga kupoteza msimu huu wa 2021/22 kwa kuwa bado haijapoteza.

Kama itasepa na pointi moja itakuwa na kazi ya kusaka pointi moja mbele ya Mbeya City katika mchezo wao ujao wa ligi.

Kwa mujibu wa Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema wanatambua mchezo wa leo utakuwa mgumu ila watapambana kupata pointi tatu ili waweze kuwa mabingwa.

“Coastal Union sio timu ya kubeza,moja ya timu imara na yenye ushindani mkubwa,ikiwa tutashinda itatufanya tuweze kutwaa ubingwa wa 28 jambo ambalo tunahitaji liwe hivyo kwa sasa,” amesema.