KOCHA Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta hajapenda kuona timu hiyo ikienda kwa kasi ya taratibu kuwania kuinasa saini ya Gabriel Jesus.
Arteta ana hofu huenda akaikosa saini ya nyota huyo wa Manchester City ambayo ni muhimu kwake kwa ajili ya msimu ujao.
Usajili uliopita Arteta alitumia pauni milioni 150 kukamilisha usajili wa Ben White,Aaron Ramsdale na Martin Odegaard.
Kuelekea msimu ujao wa 2022/23 Arteta anahitaji kuimarisha zaidi kikosi chake ambacho kitashiriki Europa League na anahitaji kumsajili mshambuliaji ambaye ni Jesus.
Hofu ya Arteta kumkosa nyota huyo inatokana na dau ambalo linahitajika kutajwa kuwa ni pauni milioni 50 huku Chelsea na Tottenham nazo zikitajwa kuwania saini ya mchezaji huyo.