HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesesema kuwa bao alilofuga Feisal Salum mbele ya Simba ni la viwango vikubwa na thamani yake ni bilioni.
Feisal alifunga bao hilo kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba na kuwaondoa Simba kwenye hatua ya nusu fainali.
Manara amesema halikuwa bao jepesi kwa kuwa kila mmoja ameona namna kazi ilivyokuwa jambo linalostahili pongezi.
“Ni bao lenye thamani kubwa ambayo inafika bilioni, shukrani kwa kazi ambayo ameifanya na tuna amini kwamba mambo yatazidi kuwa mazuri kwenye kazi yetu.
“Kikubwa kwa mashaiki kuwa watulivu wakati huu na tunaendelea kupambana kwenye mechi zilizobaki na kombe hili la shirikisho tunalihitaji pia,” amesema.
Yanga itacheza hatua ya fainali na Coastal Union ambaye imeshinda mbele ya Azam FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Bao hilo liliwafanya mastaa wa Yanga ikiwa ni pamoja na Fiston Mayele na Moloko kucheza kwa furaha.