LEO ni nusu fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo watani wa jadi Yanga na Simba wanatarajiwa kumenyana kwenye mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa.
Hamna namna mshindi lazima apatikane na tunajua kwamba kila timu imefanya maandalizi vizuri kwa ajili ya mchezo huu muhimu.
Atakayeshinda leo anauhakika wa kucheza fainali na huko pia ni muhimu kila mmoja akafanya vizuri kwenye maandalizi ili aweze kupata kile ambacho anastahili.
Ushindi kwenye mechi za hatua ya robo fainali zimewafungulia njia ya kuweza kucheza nusu fainali hivyo tuna amini kwamba kila timu imefanya maandalizi mazuri.
Wakati Yanga na Simba wakiwa Mwanza, Azam FC wao watasaka ushindi mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Kwa namna ambavyo eneo la kuchezea limekuwa na unafuu tofauti na msimu uliopita ni rahisi kupata mshindi wa maana ambaye atakuwa hasa visingizio kwa yule atakayemshinda.
Unapozungumzia fainali na nusu fainali ni michezo yenye hadhi kubwa hivyo na sehemu ya kuchezea lazima iwe na hadhi,kupelekwa Arusha kwa fainali ni jambo kubwa hivyo muhimu kuboresha mazingira yawe rafiki.
Wachezaji wacheze kwa nidhamu kwani ni muda ambao utakuwa wa kufunga jumlajumla msimu wa 2021/22 na baada ya hapo msimu mpya utakuwa unasubiriwa.
Hapa ndipo ambapo wachezaji wanakwenda kuonyesha uwezo wao na mbinu za makocha zitaonekana kwa kuwa mchezo wa mtoano hapo ni mwendo wa hesabu.