AZAM FC WAIFUATA COASTAL UNION ARUSHA

 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa wachezaji wao wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Coastal Union.

Leo Mei 26 kikosi hicho kimeanza safari kuelekea Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo wa mwisho uliopita Azam FC iliweza kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mabatini na mtupiaji alikuwa n Rodgers Kola mwenye mabao 8 ndani ya ligi.

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari wa ajili ya mchezo huo na watapambana kupata ushindi.

“Tunakwenda kucheza na wapinzani ambao ni wana timu nzuri na tuna waheshimu kikubwa ni kwenda kutafurta ushindi, mashabiki waweze kuwa pamoja nasi hatutawaangusha.

“Kila kitu kipo sawa na tunakwenda kufanya vizuri kwa kuwa tunahitaji kutwaa kombe ambalo ni la heshima na lina thamani kwetu,” amesema.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei 29 na mshindi wa mchezo huo atacheza na mshindi wa mchezo kati ya Yanga na Azam FC kwenye fainali.

Utachezwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao utatumiwa pia kwenye mchezo wa fainali.