WAAMUZI wa mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba tayari wamewekwa wazi leo.
Ni Ahmed Arajiga kutoka Manyara atakuwa mwamuzi wa kati kuweza kusimamia sheria 17 za mchezo huo.
Pia Mwamuzi msaidizi atakuwa Frank Komba na mwamuzi msaidizi namba 2 ni Mohamed Mkono huku yule wa akiba akiwa ni Elly Sasii wakati mtathimini waamuzi atakuwa Victor Mwandike.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imemtaja Keneth Pesambili kuwa kamishna wa mchezo huo.
Kwa upande wa Ofisa Habari wa mchezo huo atakuwa ni Clifford Ndimb