MSHAMBULIAJI wa Klabu ya PSG, Kylian Mbappe raia wa Ufaransa amesema kuwa Liverpool walihitaji saini yake ili kuweza kumpata.
Mbappe ambaye tayari ameshazima tetesi zote kwa kusaini dili jipya ndani ya PSG amesema kuwa aliwahi kuzungumza na Liverpool kwa ajili ya kuweza kucheza hapo.
“Tulizungumza kidogo,(Liverpool) lakini siyo sana, tulizungumza kidogo.
Mbappe amefunguka kuwa Liverpool ndiyo klabu anayoipenda mama yake,Fayza Lamari.
“Nilizungumza na Liverpool kwa sababu ni klabu pendwa ya mama yangu mama yangu anaipenda Liverpool sijui kwa nini nitamuuliza mwenyewe,” amesema