KASI NZIMA YA BIASHARA UNITED V YANGA ILIKWENDA NAMNA HII

NYOTA wa Yanga Fiston Mayele amezidi kutetema baada ya jana kufunga bao lake la 14 ndani ya Ligi Kuu Bara mble ya Biashara United kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ilikuwa ni Mei 23 ambapo mchezo huo ulikuwa ni kasi kubwa dk 45 za mwanzo zilimeguka bila timu hizo kufungana.

Katika mchezo huo timu zote ziliweza kutoshana nguvu kwa kufungana  bao 1-1 na kuwafanya waweze kugawana pointi mojamoja ndani ya ligi ikiwa ni mzunguko wa pili.

Bao la Mayele alipachika dk ya 74 kwa pigo la kichwa kilichomshinda kipa namba mbili wa Biashara United, Daniel Mgore.

Iliwachukua dk 5 Biashara United kuweka usawa bao hilo baada ya kufunga dk ya 77 kupitia kwa Collins Opare ambaye alitulia akiwa ndani ya 18 na kupiga shuti lililozama nyavuni na kumshinda kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery.

Katika mchezo huo Yanga iliweza kupiga jumla ya kona 9 ambapo miongoni mwa waliopewa kazi ya kupiga kona hizo alikuwa ni Chico Ushindi huku Biashara United wakipiga kona mbili ambazo hazikuleta matunda.

Yanga inafikisha pointi 64 ikiwa nafasi ya kwanza huku Biashara United ikifikisha pointi 24 nafasi ya 14.