FT:BIASHARA UNITED 1-1 YANGA

DAKIKA 90 Uwanja wa CCM Kirumba zimekamilika kwenye moja ya mchezo mzuri wa Ligi Kuu Bara kati ya Biashara United v Yanga na wote kuweza kutoshana nguvu.

Ubao umesoma Biashara United 1-1 Yanga ambapo walianza kufunga Yanga kisha Biashara United wao wakaweka usawa.
Ilikuwa ni bao la dk ya 74 Fiston Mayele ambaye amefikisha jumla ya mabao 14 sawa na George Mpole wa Geita Gold ambaye ni mzawa.
Bao la Biashara United lilifungwa na Collins Opare ilikuwa dk ya 77 na kufanya ubao usome 1-1 katika mchezo wa leo Mei 23.

Vivier Bahati, Kocha Mkuu wa Biashara United amesema wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata kwenye mchezo wa leo.