MANCHESTER City wameweza kutetea taji lao la Ligi Kuu England baada ya kuweza kupindua meza mbele ya Aston Villa.
Katika dakika 45 za mwanzo Aston Villa walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0 lakini kipindi cha pili waliweza kushuhudia wakifungwa mabao 3-2 na kuifanya City kufikisha pointi 93 ndani ya Ligi Kuu England.
Liverpool wao wameshinda mabao 3-1 ugenini dhidi ya Wolves na wanaishia nafasi ya pili wakiwa na pointi 92 wote wakiwa wamecheza mechi 38.