VIDEO:SHIME:KILA KITU KINAWEZEKANA,TAYARI KWA MAPAMBANO LEO

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Wasichana U17 Serengeti Girls, Bakari Shime amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Cameroon.

Shime amebainisha kwamba wanatambua uimara wa wapinzani wao hasa kutokana na mafanikio ambayo wameyapata lakini hilo haliwapi tabu kwa kuwa kwenye mpira kila kitu kinawezekana.