ARTETA AMECHOKA KUWATETEA WACHEZAJI

 MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa walistahili kupata ushindi kwenye mchezo wao dhidi ya Newcastel United.

Arsenal ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Newcastle United kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa St James Park.

Kichapo hicho kimeifanya timu hiyo kuwa kwenye wakati mgumu katika kusaka nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwania nafasi hiyo na Tottenham.

Arteta anasema :”Ilikuwa ngumu sana. Kikawaida siwezi kukaa hapa na kuanza kuwatetea wachezaji kwa walichofanya uwanjani sio rahisi.

“Siku zote nimekuwa nikiwatetea lakini hapana sasa inatosha,wapinzani wetu walikuwa bora kwetu na tangu mchezo unaanza mpaka unakamilika likuwa ngumu kukubali kwani mambo mengine huwa yanakuwa hivyo,”.