LIVERPOOL imepindua meza kibabe mbele ya Southampton iliyo nafasi ya 15 na pointi 40 kibindoni.
Nathaniel Redmond aliwatungua Liverpool mapema kabisa ilikuwa ni dk ya 13 kisha Takumi Minamino dk ya 27 aliweka usawa ilikuwa kwa shuti kali lililomshinda kipa kwenye mchezo huo.
Dakika 45 za mchezo zilikamilika kwa timu zote kufungana bao 1-1 na kumfanya Jurgen Klopp kurejea uwanjani kipindi cha pili na makakati mpya.
Dakika ya 67 kazi ilimalizwa na kijana Joel Matip na kufanya ubao wa Uwanja wa St Marys kusoma Southampton 1-2 Liverpool.
Licha ya ushindi huo bado Liverpool inabaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa na pointi 89 na vinara ni Manchester City wenye pointi 90 wote wamecheza mechi 37.