KLOPP AKIRI KUWA WALIKUWA WANAMHITAJI MBAPPE

 KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp ameweka wazi kwamba walikuwa na mpango wa kuinasa saini ya nyota wa PSG, Kylian Mbappe.

Klopp amebainisha kwamba wao sio vipofu kwenye kuingia vita vya kusaka saini yake kwa kuwa kuna timu zenye nguvu kubwa.

Klopp ameweka wazi kwamba kwa sasa hawawezi kushindana na Real Madrid pamoja na mabosi wa mchezaji huyo PSG kwenye msako wa saini yake.

Mkataba wa Mbappe na PSG unakaribia kumeguka mwezi ujao na wakati wowote atatoa maamuzi wapi atakuwa kama atabaki hapo ama atakwenda kupata changamoto mpya.

Ripoti zinaeleza kuwa Liverpool iliwahi kuhitaji saini ya nyota huyo lakini ikashindikana kuipata saini yake.

“Ni kweli tulitaka kumsajili Mbappe, ila sisi sio vipofu, tulimpenda na tulitamani awe hapa lakini hatuwezi kupambana vita vikali.

“Kuna klabu ambazo zipo kwenye mbio za kusaka saini yake na hatuwezi kushindana nao ila yeye ni mchezaji bora kabisa,”