KICHUYA AINGIA ANGA ZA SIMBA

IMEELEZWA kuwa mabosi wa Simba wanafikiria namna ya kuweza kumrudisha nyota wao wa zamani ndani ya kikosi hicho Shiza Kichuya ambaye kwa sasa anakipiga Namungo FC.

Kichuya aliwahi kucheza Simba ambapo alijiunga na timu hiyo Julai 2016 kisha akasepa 2019 kuelekea Misri na akarudi tena ndani ya Simba Januari 15,2020 mwanzoni mwa msimu wa 2020/21 akaibuka ndani ya Namungo.

Kwa sasa ni chaguo la kwanza ndani ya Namungo FC akiwa ni miongoni mwa wachezaji waliomtungua Diarra Djigui wa Yanga kwenye mchezo wa ligi.

Bao lake hilo alikuwa nje ya 18, Uwanja wa Mkapa na alifunga kwa kutumia mguu wake wa ushoto.

Pia kwenye mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Ilulu, Kichuya aliweza kutoa pasi ya bao kwa pigo la kona na ilifungwa na Jacob Masawe.

Habari zimeeleza kuwa jina lake ni miongoni mwa majina ya wachezaji ambao wanajadiliwa ndani ya Simba.

Mwenyekiti wa Simba, Murtanza Mangungu hivi karibuni alisema kuwa kwa sasa sio wakati wa usajili.