SIMBA YALIPA KISASI MBELE YA KAGERA SUGAR YAICHAPA 2-0

LEO Mei 11,2022 mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamelipa kisasi cha kutunguliwa mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.

Ushindi wa mabao 2-0 ambao wameupata leo wamelipa kisasi cha mzunguko wa kwanza baada ya Hamiss Kiza kuweza kumtungua bao 1-0 Aishi Manula walipokutana.

Leo wamekutana kwenye mzunguko wa pili na Kiza aliweza kuanza kikosi cha kwanza na kipindi cha pili Kocha Mkuu, Francis Baraza aliweza kumfanyia mabadiliko.

likuwa ni moja ya mchezo mzuri leo kwa mashabiki ambao walijitokeza kushuhudia burudani ya ligi kutokana na timu zote kucheza mpira wa pasi bila nguvu nyingi.

Hata wale waliokuwa wakitazama kupitia Azam TV kuna burudani nzuri wameipata.

Ni Kibu Dennis alianza kupachika bao la kuongoza ilikuwa dk ya 14 na John Bocco alipachika bao dk ya 30 yalitosha kuipa pointi tatu Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Ushindi huu unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 49 nafasi ya pili huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 7 na pointi 29.