LEWANDOWSKI WA ACHA TU HUKO UEFA

NOVEMBA 2,2021, Robert Lewandowski aliweka rekodi ya kuwa miongoni mwa wachezaji waliofunga na kutoa pasi ya bao pamoja na kukosa penalti kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

 

Mara ya mwisho ilikuwa ni Novemba 2013 kufanyika jambo hilo alikuwa ni Diego Costa alipofanya hivyo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lewandowski alifanya hivyo wakati timu yake ya Bayern Munich ikishinda mabao 5-2 dhidi ya Benfica katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Allianz Arena.

Katika mchezo huo Lewandowski alisepa na mpira wake kwa kuwa alitupia mabao matatu ilikuwa dakika ya 26,61 na 84 huku mabao mengine yakitupiwa na Serge Gnabry dakika ya 32 na Leroy Sane dakika ya 49.

Kwa upande wa Benfica ni Morato alitupia dakika ya 38 na Darwin Nunez alitupia bao ilikuwa dakika ya 74.

Mbali na ushindi ambao waliupata Bayern Munich waliweza kupiga jumla ya mashuti 24 na katika hayo 12 yalilenga lango huku wapinzani wao wakipiga mashuti 7 na katika hayo ni mawili pekee yalilenga lango.

Kwa upande wa pasi, Bayern Munich walipiga pasi 643 na Benfica walipiga pasi 335 hali iliyowafanya wamiliki mpira kwa asilimia 34 huku Bayern wakiwa na umiliki wa asilimia 66.

Katika kundi E walililopo Bayern Munich wamewapoteza kwa rekodi pia vigogo Barcelona kwa kuwa wao wapo nafasi ya kwanza na pointi 12 huku Barcelona wakiwa nafasi ya pili na pointi 6.

Ukiitazama ile safu ya ushambuliaji ya Bayern Munich imetupia mabao 17 katika mechi nne huku Barcelona wakiwa wametupia mabao mawili wakizidiwa na safu ya ushambuliaji ya Benfica iliyotupia mabao matano ikiwa nafasi ya tatu na pointi nne.