MORRISON,MKUDE,KUIKOSA KAGERA SUGAR

VIUNGO wa Simba wanne leo wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Mkapa mbele ya Kagera Sugar.

Mchezo wa leo ni wa mzunguko wa pili baada ya ule wa mzunguko wa kwanza Kagera Sugar kuwatungua bao 1-0 Simba, Uwanja wa Kaitaba.

Pablo Franco, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna wachezaji ambao wakosekana kwenye mchezo huo katika eneo la kiungo.

“Mkude,(Jonas),Morrison,(Bernard),Kanoute,(Sadio) na Lwanga,(Taddeo) hawa wataukosa mchezo kwa kuwa bado hawajawa fiti na ni majeruhi.

“Lakini kuwakosa hawa haina maana kwamba hawatakuwepo wengine, wapo wachezaji ambao tumewaandaa kwa ajili ya mchezo wetu huo muhimu.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kuweza kushuhdia mchezo wetu huu ambao utakuwa na ushindani mkubwa,”.