KAGERA SUGAR YATUMA UJUMBE HUU SIMBA

BUBERWA Birikes, Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar amesema kuwa watafanya kazi kubwa kupata ushindi mbele ya Simba kesho kwenye mchezo wa ligi.

Kesho Mei 11, Kagera Sugar ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Simba kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Saleh Jembe,Birikes amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Simba utakuwa ni mgumu hivyo watapambana kupata pointi tatu.

“Tunajua kwamba mchezo wetu dhidi ya Simba utakuwa ni mgumu nasi tunahitaji pointi tatu hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kuweza kupata matokeo.

“Kikubwa ambacho tunajua ni kwamba Simba ni timu kubwa lakini nasi tupo kwenye ushindani na tunahitaji pointi tatu hasa ukizingatia kwamba tumetoka kupoteza mbele ya Geita Gold,” amesema.