VIGOGO wa Kariakoo, msimu wa 2021/22 wamekwaa kisiki cha mpigo Ilulu mbele ya Namungo kwa kushindwa kusepa na pointi tatu mazima.
Msimu huu ushindani umekuwa ni mkubwa na kila timu imeoneana kufanya vizuri katika mechi ambazo inacheza jambo ambalo limekuwa likileta burudani mwanzo mwisho.
Vigogo wa Kariakoo, Yanga na Simba walipofunga safari mpaka Ilulu, walikwama kupata pointi tatu zaidi ya kuishia kuvuna pointi mojamoja kila mmoja.
Ilianza Yanga kupata pointi moja kama ilivyofanya msimu wa 2020/21 kisha ikafuata Simba kuambulia pointi moja ikitibua rekodi yakusepa na pointi tatu msimu wa 2020/21.
Timu zote mbili ziliambulia sare ya kufungana katika mechi zao ambazo walicheza Uwanja wa Ilulu,mbele ya Namungo FC.
Namungo 1-1 Yanga kisha mchezo wa Simba ilikuwa Namungo 2-2 Simba huku staa Obrey Chirwa akizitungua timu zote hizo mbili zilipotua Ilulu.