FT: YANGA 0-0 SIMBA

DAKIKA 90 zimekamilika Uwanja wa Mkapa kwa ubao kusoma Yanga 0-0 Simba.

Ulikuwa ni mchezo mkali wa mzunguko wa pili na kufanya dk 180 kukamilika bila kufungana.

Ule wa awali,ubao ulisoma Simba 0-0 Yanga hivyo katika msako wa pointi 6 wamegawana pointi mbilimbili.

Mwamuzi wa kati Ramadhan Kayoko alionekana kuwa na presha mwanzo kabla ya mwisho kutulia na kwenda sawa na mwendo wa mchezo ambao ulikuwa ni wa kasi.

Sare hii inawafanya Yanga wabaki namba moja na hawajafungwa mchezo wowote kwa msimu wa 2021/22 katika mechi 21 ambazo wamecheza.

Kibindoni sasa wanafikisha pointi 55 huku Simba ambao ni mabingwa watetezi wakiwa na pointi 42 baada ya kucheza mechi 20.