KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa leo kati ya Yanga v Simba, vinara wa Ligi Kuu Bara, wametaja idadi ya mabao ambayo wanaamini watashinda.
Vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 54 na wamecheza mechi 20 wanafuatiwa na Simba ambao ni mabingwa watetezi wakiwa na pointi 41 baada ya kucheza mechi 19.
Ni mchezo wa mzunguko wa pili ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ambapo ule wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Simba 0-0 Yanga.
Hassan Bumbuli,Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanaamini wanaweza kuwafunga wapinzani wao wa leo na kuodoka na pointi tatu muhimu.
“Kama itakuwa hivi ninadhani labda itakuwa wenyeji 2, (Yanga) na wao 0, (Simba) kwenye mchezo wetu wa dabi ambao utachezwa Uwanja wa Mkapa.
“Wakijitahidi sana kwenye mchezo wetu labda itakuwa 2-1 ila ambacho ninajua ni kwamba tunakwenda kwenye mchezo tukiamini kwamba tunacheza na timu kubwa na yenye wachezaji wazuri,”.