PSG WAGAWANA POINTI NA STRASBOURG

WAKIWA Uwanja wa de la Meinau wababe PSG waligawana pointi mojamoja na Strasbourg katika mchezo wa Ligue 1.

Ilikuwa ni mabao ya Kevin Gameiro dk 3 Marco Verralti alijifunga dk 75 na bao la usiku lilifungwa na Anthony Caci dk 90+2.

Kwa wababe PSG wao walifunga kupitia kwa Kylian Mbappe aliyetupia mabao mawili ilikuwa dk 23 na 68 huku Achraf Hakimi akitupia bao moja dk ya 64.

Kwenye msimamo PSG inafikisha pointi 79 baada ya kucheza mechi 35 huku Strasbourg ikiwa nafasi ya 5 na pointi 57 baada ya kucheza mechi 35.