KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amepanga kubadilisha mbinu dhidi ya Simba kutokana na ubora wa watani wao hao wa jadi.
Kauli hiyo aliitoa mara baada ya Yanga kuingia kambini mapema wiki hii kujiandaa na mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Nabi amesema katika mchezo huo, wanakwenda kukutana na timu kubwa, hivyo ni lazima wacheze kwa kuwaheshimu ili wapate matokeo mazuri.
Nabi amesema Simba ina wachezaji wengi wa kimataifa ambao ni bora kama ukifanya makosa, basi lazima watakuadhibu.
Aliongeza kuwa, katika mchezo huo wataingia tofauti kwa maana ya kimbinu na mfumo watakaoutumia ambao ni wa kucheza kwa kuiheshimu Simba.
“Tulivyocheza michezo iliyopita ya ligi dhidi ya Namungo na KMC ni tofauti tutakavyocheza dhidi ya Simba, hivyo ni lazima tuingie uwanjani kwa mbinu tofauti za kuwaheshimu zaidi.