SIMBA YATAJA MAMBO YANAOITESA TIMU HIYO

KOCHA Mkuu wa Simba, Raia wa Rwanda, Thierry Hitimana amefunguka mambo matatu yanayosababisha
washindwe kufanya vizuri 
tangu kuanza kwa msimu huu.


Hitimana amefichua 
mambo hayo kufuatia Simba kucheza mechi nne katika Ligi Kuu Bara ambapo imefanikiwa
kushinda mechi 
mbili na kutoka sare mechi mbili huku ikiwa ya katika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi
kuu ikiwa pointi 
nane.

“Tuna mambo matatu ambayo tunapitia lakini jambo la kwanza presha imekuwa kubwa ingawa ni kawaida katika soka lakini kwetu imekuwa kubwa kwa sababu tumekuwa na matokeo mabaya ambayo mashabiki wa Simba hawakutarajia kwa kuwa msimu uliopita walikuwa hawajayazoea maana msimu uliopita timu ilikuwa juu sana.


“Lakini kukosekana kwa 
wachezaji kama Clatous Chama na Luis Miquissone wao walisaidia kwa sehemu
kubwa Simba kufanya 
vizuri ukiangalia kwa nafasi ambazo wanacheza, Chama atacheza kumi na Miquissone 11 ambao walisaidia ila sasa wengi bado wapya hivyo shida ipo ambayo itakuwa ya mpito kwetu.


“Ukiangalia tuna 
wimbi kubwa la wachezaji ambao wapo majeruhi, mtu kama Chris Mugalu hayupo, Lwanga
hayupo ambao 
hao wanaanza kwenye kikosi hali ambayo inatulazimu kuwatumia wachezaji wengi ambao wanakaa benchi na kuendelea kujipanga ili tufanye vizuri ikiwemo mechi yetu dhidi ya Namungo,” alisema Hitimana.


Leo Jumatano, 
Simba inatarajia kucheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo katika mchezo
ambao utapigwa kwenye 
Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.


Akizungumza na 
Championi Jumatano, Hitimana alisema kuwa, wanapitia wakati mgumu kwa sasa kutokana na timu yao kukwamishwa na uwepo wa mambo matatu ambayo hayakuwepo katika msimu uliopita hali iliyopelekea kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi Kuu.