FISTON Mayele, mshambuliaji namba moja ndani ya Ligi Kuu Bara amesema kuwa mchezo ujao dhidi ya Simba anaamini kwamba akipewa nafasi atafunga.
Simba inayonolewa na Kocha Mkuu,Pablo Franco ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Yanga, Aprili 30 kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Kwenye msimamo Yanga inaongoza ikiwa na pointi 54 inatarajiwa kukutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi zao ni 41.
Mayele mwenye mabao 12 na pasi tatu za mabao amesema kuwa anaamini kwamba mchezo wao utakuwa na ushindani mkubwa lakini wanachohitaji ni ushindi.
“Tunatambua kwamba mchezo wetu utakuwa na ushindani mkubwa lakini ambacho tunahitaji ni matokeo hilo lipo wazi na tutapambana kupata ushindi,”.
Mchezo uliopita mbele ya Namungo FC, Fiston Mayele aliweza kufunga na pia aliwafunga Azam FC walipokutana kwenye mzunguko wa pili na ule wa kwanza.