KIMATAIFA:ORLANDO 0-0 SIMBA

MCHEZO wa Kombe la Shirikisho kwa sasa hatua ya robo fainali ambapo wawakilishi wa Tanzania Simba wapo kazini ni mapumziko.

Dakika 45 za mwanzo zimekamilika huku ubao ukisoma Orlando Pirates 0-0 Simba.

Licha ya Simba kutokufungwa bado wapo kwenye ugumu mkubwa wa kushambuliwa kwa kasi na wapinzani wao.

Chris Mugalu yupo kwenye ulinzi mkubwa na Simba hawajapiga shuti hata moja ambalo limelenga lango.

Timu zote zinapambana kuweza kukata tiketi ya kutinga hatua ya nusu fainali kwenye Uwanja wa Orlando,Afrika Kusini.