BINGWA wa Dunia mara 7 katika mashindano ya uendeshaji wa magari ya Langalanga maarufu kama Formula 1 Sir Lewis Hamilton pamoja na Bingwa namba moja katika mchezo wa tenesi kwa wanawake Serena Williams kwa pamoja wameweka kitita cha Paundi milioni 20 ili kuwa wamiliki wapya wa Klabu ya Chelsea.
Wanamichezo hao maarufu wameingia ubia kwa kuungana na mwekezaji anayetajwa kuwa na nafasi kubwa ya kuwa mmiliki mpya wa klabu ya Chelsea Sir Martin Broughton.
Muendesha magari ya Langalanga na bingwa wa dunia mara saba katika mchezo huo Sir Lewis Hamilton kwa sasa anaendesha magari ya Kampuni ya Mercedes ambapo kipindi cha nyuma alikuwa akifanya kazi na Kampuni ya Mclaren kuanzia kipindi cha mwaka 2007-2012.