RALF AFUNGUKIA JUU YA KOCHA MPYA NA POGBA

KOCHA wa muda ndani ya kikosi cha Manchester United Ralf Rangnick amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumza kuhusu hatma ya kiungo wa timu hiyo Paul Pogba.

Wakati huo pia Rangnick anaamini kwamba Erik ten Hag ambaye amepewa kandarasi ya kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo ni moja ya makocha wazuri ambao United imewapata.

“Nina uhakika kwamba ni moja ya makocha wazuri,ila siwezi kusema kwa uhakika ni jambo gani ambalo linaweza kutokea kwake.

“Kuhusu Pogba mimi siwezi kuzungumzia jambo kwani muda huu yeye ni majeruhi lakini nina amini kwamba ni mchezaji mzuri ambaye ameshinda taji la Kombe la Dunia akiwa timu ya Taifa ya Ufaransa.

“Kwa namna ambavyo yupo ni moja ya aina ya wachezaji wazuri lakni acha kwa hilo nikae kimya amekuwa akipambana kwenye mechi ambazo tunacheza kuonyesha uwezo mkubwa.

“Kwa msimu huuu hiyo haiwezi kuwa kesi kwake kwa msimu huu, imekuwa hivyo kwa miaka ya hivi karibuni,”.