KOCHA KAIZER CHIEFS AFUKUZWA KAZI

KLABU ya Kaizer Chiefs na Kocha Stuart Baxter wamefikia makubaliano ya pamoja ya kuvunja mkataba wa kocha huyo aliyerudi kuifundisha klabu hiyo kwa mara ya pili mara baada ya kuhudumu mwanzo kwenye klabu hiyo.

Akiwa na Kaizer Chief amefanikiwa kushinda michezo 9 ametoka sare michezo 6 na kufungwa michezo 8 na katika kipindi hicho klabu imefunga jumla ya mabao 25 huku ikiruhusu kufungwa mabao 23 kitendo ambacho kimepelekea mabosi wa Kaizer Chiefs kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.

Kocha Msaidizi Arthur Zwane pamoja na Dillon Sheppard watachukua mikoba hiyo hadi mwisho wa msimu huku mchezo unaofuata ukiwa ni dhidi ya Stellenbosch Jumamosi ya Aprili 23 mwaka huu.