AZAM FC YAIZIMA GEITA GOLD USIKU

KIKOSI cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina usiku wa kuamkia leo Novemba 3 kilisepa na pointi tatu mazima mbele ya Geita Gold.

 

Ni kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 1-0 Geita Gold.

Bao la ushindi lilipachikwa na mshambuliaji wao Rodgers Kola ilikuwa dakika ya 81 itazama mazima kwenye nyavu.

Mchezo huo ulichezwa usiku na Azam FC ikaizima Geita God usiku zikiwa zimeaki dakika 8 mchezo kukamilika.

Sasa Azam FC inafikisha pointi 7 ikiwa nafasi ya 7 huku Geita Gold ikiwa nafasi ya 14 na pointi mbili na zote zimecheza mechi tano.