HIZI HAPA KUKIWASHA LEO LIGI KUU ARA

NI Aprili 6 Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea ambapo mechi mbili zinatarajiwa kuchezwa kwenye viwanja viwili tofauti kwa timu kusaka pointi tatu muhimu.

Uwanja wa Karume, Mara unatarajiwa kuchezwa mchezo kati ya Biashara United v Mbeya Kwanza ya kutoka Mbeya.

Biashara United imekusanya pointi 19 inakutana na Mbeya Kwanza yenye pointi 14 zote zimecheza mechi 18.

Mchezo mwingine ni ule utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku ambapo itakuwa ni Dar Dabi.

Azam FC V Yanga ambao ni vinara wa ligi na Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ile ya pili ikiwa mikononi mwa Simba ambao ni mabingwa watetezi.