KIMATAIFA MAKOSA YASIPOREKEBISHWA SAFARI ITAISHIA NJIANI

    HATUA moja kila wakati hasa kwa wawakilishi wetu wa Tanzania kwenye mechi za kimataifa baada ya kuweza kutimiza lengo la kufika hatua ya robo fainali.

    Tulizungumza hapa kwamba haitakuwa kazi nyepesi kwa kuwa wapinzani wao USGN hawakuwa na cha kupoteza na ilikuwa hivyo kwa kuwa walicheza mchezo ambao ulikuwa ni wa tofauti.

    Dakika 45 za mwanzo Simba ilicheza mpira mzuri ila ilikosa jambo moja la msingi utulivu na kutumia nafasi ambazo wanazipata.

    Nilizungumza hapa kwamba kinachoweza kuwaongezea hali ya kujiamini ni kupata mabao ya mapema ila haikuwa hivyo waliweza kufanya makosa kwenye kutumia nafasi.

    Labda kama wangeweza kutumia nafasi ambazo walizipata kipindi cha kwanza ingekuwa rekodi mpya kwa ushindi mkubwa kimataifa kwao.

    Haikuwa hivyo kwa kuwa waliweza kubadilika kipindi cha pili na kutumia makosa ambayo waliyatengeneza wapinzani wao.

    Hili ni kubwa sana na linastahili pongezi kwa wachezaji na benchi la ufundi hivyo yale makosa ya kushindwa kutumia nafasi hilo linawahusu wachezaji lazima lifanyiwe kazi.

    Mashuti 20 ambayo walipiga Simba sio machache hasa kwa timu inayosaka ushindi na kupiga mashuti 6 pekee langoni hili ni tatizo ambalo lipo linahitaji kufanyiwa kazi.

    Yote haya ni kuweza kuona kwamba kwenye hatua ya robo fainali lile tatizo la kutumia nafasi ambazo zinatengenezwa linatatuliwa.

    Kama mwendo utakuwa huu kwenye mechi zijazo basi tutarajie kuona kikomo kwa Simba kuwa hatua ya robo fainali jambo ambalo halitakuwa na afya kwa soka letu.

    Mipango makini na utulivu kwa wachezaji ni muhimu kwenye kila mechi bila kujali inawezekana vipi kupenya hatua hii kubwa na kufanya vizuri.

    Inawezekana na ipo njia kwa Simba kutinga hatua ya nusu fainali lakini mpaka waweze kufanyia kazi makosa ambayo wameyafanya.

    Katika hatua ya robo fainali hapa sio pointi tena bali ni idadi ya mabao hapa ugumu huwa unakuwa kwa Simba kupata ushindi ugenini kwenye hatua hii ya robo fainali.

    Ipo wazi kwamba kimataifa kwa Afrika kila mtu ashinde mechi zake za nyumbani hapo lazima Simba wajipange na kujituma zaidi na zaidi kupata matokeo ugenini.

    Nina amini kwamba kwa sasa watakuwa wanajua ambacho wanapaswa kukifanya kwenye hatua ya robo fainali ambayo huwa inakuja kwa mtindo wa kipekee.

    Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa, fanyeni kweli na inawezekana kwa kuwa muda ni sasa.

    Dizo_Click.

    Previous articleHIZI HAPA KUKIWASHA LEO LIGI KUU ARA
    Next articleBOSI YANGA AWEKA WAZI KUWA MAYELE ATAFUNGA SANA