MOLOKO,NGUSHI WAREJEA KUIVAA AZAM FC

CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga amesema kuwa kuna wachezaji ambao wamerudi kwenye kikosi baada ya kuwa nje kwa muda kutokana na kutibu majeraha.

Kesho Yanga inatarajiwa kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC ambao nao pia waazihitaji pointi hizo.

Kaze amesema:”Wapo baadhi ya wachezaji walikuwa nje kutokana na majeruhi lakini kwa sasa wameanza mazoezi ikiwa ni pamoja na Jesus Moloko amerudi na jana ameanza mazoezi na wenzake ametoka kwenye mazoezi ya utimamu wa mwili na sasa anafanya mazoezi na wenzake.

“Kweli utimamu wake wa mwili haujawa asilimia 100 ila anaweza kuwa vizuri tutaangalia hali yake leo na kuna wengine ambao wanaweza kuanza.

“Abdul Shaibu,’Ninja’ naye pia amerudi aliweza kucheza mbele ya Mafunzo pia Crispin Ngushi naye amerudi hivyo tuna amini kwamba tutaongeza nguvu kwenye timu yetu,” amesema.