LEO Aprili 5 imechezwa droo ya Kombe la Shirikisho pamoja na ile ya ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa upande wa Tanzania wawakilishi ni Simba ambao walikuwa kundi D na kwenye kundi hilo wamepenya sawa na RS Berkane wote wakiwa na pointi 10.
Hivi ndivyo ambavyo kazi itakuwa:-
Simba v Orlando Pirates hii ni ya Afrika Kusini
Pyramids FC V TP Mazembe
Al Masry v RS Berkane
Al Ittihad v Al Ahli Tripoli.
Duru ya kwanza itanza kuchezwa Aprili 17,2022 huku marudiano yakipangwa kufanyika Aprili 24,2022.