BAADA YA KICHAPO KOCHA ARSENAL ASEMA NI MATOKEO MABAYA

MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa matokeo ambayo wameyapata ni mabaya hawakutarajia.

Baada ya dk 90 ubao wa Uwanja wa Selhurst Park ulisoma Crystal Palace 3-0 Arsenal.

Watupiaji walikuwa ni Jean-Phillupe Mateta dk 16,Jordan Ayew dk 24 na Wilfried Zaha dk 74 kwa mkwaju wa penalti.

Arsenal imeyeyusha pointi tatu mazima ikiwa ugenini inabaki na pointi 54 nafasi ya 5 huku Crystal Palace ikiwa nafasi ya 9 na pointi 37.

Crystal Palace imecheza mechi 30 na Arsenal wamecheza mechi 29.