DAKIKA 45 Uwanja wa Mkapa ubao Simba 0-0 USGN hatua ya makundi.
Simba wamekwama kutupia kupitia kwa Pape Sakho aliyekosa nafasi mbili, Sadio Kanoute nafasi tatu za kufunga.
Pia Kanoute kwa kucheza faulo ameonyeshwa kadi ya njano na mwingine kwa Simba ni Joash Onyango ambaye hakuwa na chaguo alimchezea faulo Adebayo Victorean.
Simba wamepiga kona 10 USGN 0 huku mashuti yakiwa 10 na moja limelenga lango.